Saturday, 1 August 2015

wagombea wa nafasi ya ubunge kupitia tiketi ya CCM jimbo la Vwawa wilaya ya Mbozi

Pichani ni msanii  wa nyimbo za asili Nyondo akitumbuiza katika kikao cha ndani ya chama katika kata ya Ilolo

Mgombea wa kiti cha ubunge ndugu Stanislaus Nsojo kupitia chama cha mapinduzi akinadi sera zake katika kikao cha ndani ya chama, kata ya Ilolo Vwawa

Pichani ni mmoja wa wagombea wakiti cha ubunge kupitia CCM ndungu John Ntenga akinadi sera zake katika kikao cha ndani kata ya Ilolo

Mwanachama wa chama cha Mapinduzi akiuliza swali kitika kikao cha ndani kata ya Ilolo

Mgombea akitoa ufafanuzi katika sera zake

Pichani mgombea wa ubunge ndugu Nducha akieleza vipaumbele vyake kwa wanachama wa ccm wa kata ya ilolo

Pichani ni mgombea akisikiliza kwa makini maswali ya wanachama cha mapinduzi kutokana na sera zake

Pichani wanachama wakiwasikiliza  wagombea wakiti cha ubunge kupitia Chama Chama CCM kwenye kikao cha ndani kata ya Ilolo


Pichani ni mmoja wa wagombea wakiti cha ubunge kupitia CCM ndungu John Hsunga  akinadi sera zake katika kikao cha ndani kata ya Ilolo


Pichani ni  wagombea wakiti cha ubunge kupitia Chama Chama CCM baada ya kikao cha ndani kata ya Ilolo

Pichani ni  wagombea wakiti cha ubunge kupitiaChama Chama CCM baada ya kikao cha ndani kata ya Ilolo

KURA ZA MAONI CCM



Kura za maoni CCM

Wagombea wa Ubunge katika jimbo la Vwawa wilayani Mbozi, kwa tiketi ya chama cha mapinduzi wamefikia tamati ya kuomba ridhaa kwa wanachama wenzao  Julai 31 mwaka huu katika kata ya Ilolo

Katika kuhitimisha zoezi hilo wagombea hao walipewa fursa ya kueleza nia zao pindi watakao pewa dhamana ya kuongoza jimbo hilo.

Akitoa  ahadi zake mgombea Stanislaus Nsojo  aliahidi  kujenga ofisi ya chama cha mapinduzi kata ya Ilolo ambayo kwa sasa haiko katika hali nzuri, na kusema kuwa  atasimamia vizuri upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu  kwa vijana na kina mama.

Vilevile mgombea Stanslaus  aliahidi kusimamia kwa makini ujenzi wa barabara na miundo mbinu mbalimbali katika kata zote kwa kushirikiana na wananchi wa Vwawa
Sanjari na hayo ndugu Nsojo alionya kuhusu utoaji wa rushwa kuwa unapoteza haki ya msingi

Kwa upande wake John Ntenga mgombea wa nafasi ya ubunge katika chama hicho alitaja mambo yaliyomsukuma kugombea kiti hicho kuwa ukosekanaji wa pembejeo kwa wakati unaowafanya wakulima kushindwa kuzalishwa ipasavyo.

Vilevile aligusia kuhusu utitili wa kodi zisizokuwa za msingi kwa wafanya biashara ambao unawavyunja moyo wafanyabiashara wengi, hivyo basi atahakikisha wafanya biashara nao wananufaika .

Aliongeza kuwa  hakuna sababu ya ukosekanaji wa Maji kwakuwa anauwezo kubuni mbinu mbadala ya kupata maji na kutatua tatizo la maji kwa mji wa vwawa

Pia kwa upande wake , mgombea Nducha  alisisitiza elimu  kwasababu ya uchache wa wasomi ndio chanzo cha umaskini hivyo basi ataboresha elimu ya msingingi, vile vile Vifaa vya michezo maana michezo ni chanzo cha ajira.

Hata hivyo Jofrey Mwashitete mtaalamu wa kilimo alisema kuwa analifahamu vizuri jimbo lake hivyo basi ataanzishwa mradi wa umwagiliaji katika wilaya ya Mbozi ili wakulima wanufaike na kilimo.

Kwa kuhitimisha zoezi hilo ngombea  Haonga alisisitiza upatikanaji wa ajira kwa vijana na kina mama, pia  kutafuta masoko ya mazao kwa wakulima, na kuboresha miundo mbinu iliiweze kufanana na hadhi ya mkoa.

Aliongeza kuwa wamchague kiongozi atakaye waunganisha na serikali ilikuwaletea maendeleo ikiwa ni kuwekea mazingira mazuri ya kibiashara.