| grey Mwakisole mjumbe wa kamati ya siasa CCM, akiwahutubia wananchi wa jimbo la Vwawa, Mkutano uliofanyika stendi ya Malori Vwawa mjini. |
Mbozi.
Idadi ya Mawaziri walioanguka katika majimbo yao imezidi kuongezeka ambapo
aliyekuwa Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi (CCM)
amebwagwa kwenye kinyang’anyiro cha Ubunge Jimbo la Mbozi na kijana Mwalimu
Pascal Haonga (Chadema).
Zambi
ambaye alikuwa akitetea nafasi hiyo kwa kipindi cha chatu katika Jimbo
hilo alijikuta akifuata nyayo za aliyekuwa ‘bosi’ wake Stephen Wasira
(CCM) aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika ambaye alibwagwa na
mwanadada Ester Bulaya (Chadema) katika Jimbo la Bunda.
Mkurugenzi
wa uchaguzi Jimbo la Mbozi, Edina Mwaigomole alimtangaza Haonga kwa tiketi ya
Chadema kuwa Mbunge Mteule wa Jimbo hilo baada ya kupata kura 36,362 akifuatiwa
na Zambi kura 34,584 na Julius Mwanitega wa chama cha Act-Wazalendo
aliyeambulia kura 732.
Katika
Jimbo la Vwawa Wilayani Mbozi, Mwaigomole alimtangaza mgombea wa CCM, Japhet
Hasunga kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo baada ya kupata kura 36,705 akiwa
‘amewapiku’ wapinzani wake Fanuel Mkisi (Chadema) aliyepata kura 35,400 na
mgombea wa Chama Cha ACT- Wazalendo aliyeambulia kura 502.
Hata
hivyo wakati wa kutangaza matokeo hayo kwa majimbo yote mawili, Zambi (CCM)
hakutokea eneo la kutangazia matokeo wala hakusaini fomu ya kukubali kushindwa
pamoja na mgombea wa Chadema, Mkisi katika Jimbo la Vwawa naye hakuweza kusaini
fomu hiyo licha ya kuwepo kwenye hadhara ya kusikiliza matokeo hayo.
Wakizungumza
kwa nyakati washindi wa majimbo hayo, Haonga, Chadema Mbozi na Hasunga wa CCM
jimbo la Vwawa walisema licha ya kuchagulia kwao kupitia vyama vyao lakini
waliowachagua sio wa chama husika bali kutokana na kila mpiga kura kumuamini
mtu anayeweza kuwawakilisha vyema hivyo na wao watafanya kazi bila ubaguzi
wowote.
Haonga
(chadema) alisema ‘Nawashukuru wananchi wa Mbozi kunipa ridhaa ya kuwa
mwakilishi wao, najua nimechaguliwa kupitia Chadema lakini walionichagua ni
wananchi wa Mbozi bila kujali itikadi ya Chama hivyo nawaahidi heshima
walionipa sitawaangusha’.
![]() |
| Mgombea udiwani kata ya Ichenjezya kupitia CCM Mkola,akiomba kura kwa wananchi wa kata hiyo |
![]() |
| Mgombea udiwani kata ya Vwawa Benard Mwazembe kupitia CCMakimuombea kura mgombea ubunge CCM Japhet Hasunga eneo la Ichenjezya- Kwajim |
![]() |
| Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi wakiwa kwenye kampeni mjini Vwawa Septemba 14 mwakja huu |
![]() |
| Mgombea wa ubunge kupitia CCM Japhet Hasunga jimbo la Vwawa akiwa kwenye kampeni akinadi sera zake kuwashawishi wananchi wa Ichenjezya kumchagua |
![]() |
| Wananchi wa kata ya Ichenjezya wakimsikiliza mgombea wa ubunge CCM jimbo la Vwawa akinadi ser |
![]() |
| Mgombea wa urais CHADEMA Edward Lowasa akiondoka Jimbo la Tunduma baada ya kuomba kura tarehe 19 Octoba 2015 |
![]() |
| Mgombea wa urais CHADEMA akiwaaga wakazi wa Tunduma baada ya kuomba kura |
![]() |
| Mgombea urais Chadema Edward Lowasa akiwanadi wagombea Udiwani Jimbo la Tunduma tarehe 19 Octoba mwaka huu |
![]() |
| Mgombea wa urais kupitia CHADEMA Edward Lowasa akisubiri kunadi sera zake kwa wananchi wa Tunduma tarehe 19 Octoba 2015 |
![]() |
| Wagombea waliotangazwa leo kushinda viti vya ubunge CHADEMA jimbo la Mbozi Pascal Haonga na Japhet Hasunga CCM jimbo la Vwawa |
![]() | |
|
![]() |
| Mgombea ubunge jimbo la Momba kwa tiketi ya ACT Weston Simwelu akionekana mwenye furaha licha ya kushindwa katika kinyan'ganyilo hicho |
![]() |
| Mgombea ubunge CCM Japhet Hasunga akilaani vikali kitendo cha uchomaji wa ofisi za CCM wilaya ya Mbozi |
![]() |
| Baadhi ya wanachama wa CCM wakiangalia jengo lao lilivyo teketezwa kwa moto na watu wasiojulikana |
![]() |
| Ofisi ya chama cha mapinduzi wilaya ya Mbozi yateketezwa kwa moto |
![]() | |
|
![]() |
| Mgombea wa urais CHADEMA akiwanadi madiwani wa UKAWA wa jimbo la Vwawa kwa wananchi wa jimbo hilo |
![]() |
| Mgombea wa ubunge CHADEMA Jimbo la Vwawa Fanuel Mkisi akitoa kero za wananchi wa Vwawa kwa mgombea wa urais kupitia chama hicho Edward Lowasa tarehe 17 Octoba 2015 |
![]() |
| Mgombea wa Ubunge CHADEMA Fanuel Mkisi akinadi sera zake kwa wananchi wa Ilembo |
![]() | |
|
![]() |
| Wananchi wa Ianzya kata ya Ipunga wakiapa kama watamchagua mgombea wa ubunge jimbo la Vwawa Fanuel Mkisi kupitia CHADEMA |
![]() | |
|
![]() |
| Mgombea wa ubunge CHADEMA jimbo la Vwawa Fanuel Mkisi akinadi sera zake katika kijiji cha Ipenzya Septemba 2, mwaka huu |
![]() |
| Mwanasheria wa CHADEMA nyanda za juu kusini akimnadi mgombea wa ubunge kwa tiketi ya chama hicho kijiji cha Ipanzya jimbo la Vwawa |
![]() |
| Wakazi wa mji wa Tunduma wakimsikiliza mgombea wa kiti cha ubunge CHADEMA Frank Mwakajoka eneo la stendi kuu Tunduma |
![]() |
| Mgombea ubunge jimbo la Tunduma akiwa kwenye kampeni eneo la Stendi Kuu mjini humo |



























No comments:
Post a Comment