Kura
za maoni CCM
Wagombea
wa Ubunge katika jimbo la Vwawa wilayani Mbozi, kwa tiketi ya chama cha
mapinduzi wamefikia tamati ya kuomba ridhaa kwa wanachama wenzao Julai 31 mwaka huu katika kata ya Ilolo
Katika
kuhitimisha zoezi hilo wagombea hao walipewa fursa ya kueleza nia zao pindi
watakao pewa dhamana ya kuongoza jimbo hilo.
Akitoa ahadi zake mgombea Stanislaus Nsojo aliahidi kujenga ofisi ya chama cha mapinduzi kata ya Ilolo
ambayo kwa sasa haiko katika hali nzuri, na kusema kuwa atasimamia vizuri upatikanaji wa mikopo yenye
riba nafuu kwa vijana na kina mama.
Vilevile
mgombea Stanslaus aliahidi kusimamia kwa
makini ujenzi wa barabara na miundo mbinu mbalimbali katika kata zote kwa
kushirikiana na wananchi wa Vwawa
Sanjari
na hayo ndugu Nsojo alionya kuhusu utoaji wa rushwa kuwa unapoteza haki ya
msingi
Kwa
upande wake John Ntenga mgombea wa nafasi ya ubunge katika chama hicho alitaja
mambo yaliyomsukuma kugombea kiti hicho kuwa ukosekanaji wa pembejeo kwa wakati
unaowafanya wakulima kushindwa kuzalishwa ipasavyo.
Vilevile
aligusia kuhusu utitili wa kodi zisizokuwa za msingi kwa wafanya biashara ambao
unawavyunja moyo wafanyabiashara wengi, hivyo basi atahakikisha wafanya
biashara nao wananufaika .
Aliongeza
kuwa hakuna sababu ya ukosekanaji wa Maji
kwakuwa anauwezo kubuni mbinu mbadala ya kupata maji na kutatua tatizo la maji
kwa mji wa vwawa
Pia
kwa upande wake , mgombea Nducha alisisitiza elimu kwasababu ya uchache wa wasomi ndio chanzo
cha umaskini hivyo basi ataboresha elimu ya msingingi, vile vile Vifaa vya
michezo maana michezo ni chanzo cha ajira.
Hata
hivyo Jofrey Mwashitete mtaalamu wa kilimo alisema kuwa analifahamu vizuri jimbo
lake hivyo basi ataanzishwa mradi wa umwagiliaji katika wilaya ya Mbozi ili
wakulima wanufaike na kilimo.
Kwa
kuhitimisha zoezi hilo ngombea Haonga
alisisitiza upatikanaji wa ajira kwa vijana na kina mama, pia kutafuta masoko ya mazao kwa wakulima, na
kuboresha miundo mbinu iliiweze kufanana na hadhi ya mkoa.
Aliongeza
kuwa wamchague kiongozi atakaye waunganisha na serikali ilikuwaletea maendeleo
ikiwa ni kuwekea mazingira mazuri ya kibiashara.
No comments:
Post a Comment