Thursday, 4 December 2014



KAMPENI ZA UCHAGUZI WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA CHAMA CHA CHADEMA KATA YA VWAWA

Ikiwa serikali imezindua rasmi kampeni za uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa Disemba Mosi mwaka huu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeanza rasimi  kampeni  hizo za kuwanadi  wagombea wao .

Katika mkutano huo Katibu Mwenezi wa chama hicho Emmanuel Zambi amewataja wagombea wanafasi za wenyeviti kuwa ni Medelina Nyondo Mtaa wa Haloli, Naomi Mwakasege Mtaa wa Vwawa kati, Elizabeth Kalago, Abrahamu Kalonge Mtaa wa Mwenge , John Mkondya Vwawa Sokoni , na Ephraim Mwakateba  mtaa wa Lami.

Emmanuel Zambi amewanadi wagombea hao kuwa ni wachapakazi na wamepewa mafunzo maalumu kuhusu serikali za mitaa na jinsi ya kuongoza serikali za mitaa kwa nia ya kuleta maendeleo pindi watakapopewa ridhaa ya kuongoza mitaa yao.

Vilevile kwa upande wake diwani wa kata ya Vwawa Richard Kibona amesema kuwa mji wa Vwawa unapanuka kwa kasi sana hivyo unahitaji miundo mbinu iliyo bora inayoweza kukukidhi viwango vya mji ilikuleta maendeleo katika mji huo kuliko hivi sasa

Kwa upande wake Dr Mgalla amesisitiza kuwa kwakipindi hiki mabadiriko ni lazima hivyo wasifanye makosa kuto kukichagua chama hicho kwasababu  kinalengo la kuwaletea mabadiriko ya hali ya juu kuliko ilivyo sasa.

 Katibu huyo ameongeza kuwa  miundombinu duni iliopo katika mji huo inasababisha ajali kila kukicha hivyo basi imefika kipindi cha mabadiriko wananchi kufanya uchaguzi ulio sahihi cha kuchagua wagombea wao.

Vilevile ndugu Amanyisye amesema kuwa michango yote inayotolewa na wananchi inatakiwa kujua idadi ya wananchi waliochangia na pesa zilizopatikana katika uchangiaji huo ilikuwabana viongozi wenye tamaa na pesa za walipakodi kwasababu kunabaadhi ya viongozi waliotafuna tayari pesa hizo .


Mmoja wa wawagombea wa nafasi za Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kata ya Vwawa.


Wananchi wa kata ya Vwawa wakiwasikiliza wagombea wa nafasi za Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wakinadi sera zao eneo la Vwawa mjini Disema 2, 2014.
Wananchi wa Kata ya Vwawa wakiwasikiliza wagombea wa nafasi za Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wakinadi sera zao eneo la Vwawa mjini Disemba 2 mwaka huu.
Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Mbozi Emmanuel Zambi akiwahutubia wananchi wa Kata ya Vwawa kwenye kampeni za uchaguzi wa Wenyeviti  wa  Serikali za Mitaa Disemba 2 mwaka huu.

Wednesday, 3 December 2014


KAMPENI ZA UCHAGUZI WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA CHAMA CHA MAPINDUZI KATA YA VWAWA
Ikiwa serikali imezindua rasmi kampeni za uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa Disemba Mosi mwaka huu Chama cha Mapinduzi (CCM) hakikubaki nyuma nacho kimeendelea na kampeni  za kuwanadi  wagombea wao zilizofanyika Tarehe 3 Disemba 2014, eneo la Ichenjezya Kitongoji cha Mbugani .

Akizungumza katika kampeni hizo katibu Tarafa mstaafu wa Vwawa Justina Kasunga amewanadi wagombea wa nafasi za wenyeviti wa mitaa kuwa ni wachapakazi na wamelelewa katika maadili ya uongozi bora hivyo wananchi wasifanye makosa kuto kuwachagua wenyeviti hao.

Aidha amesema kuwa anasikitika sana wanachama wavyama pinzani kugeuza dhana ya vyama vingi  wakidhani kupinga na kufanya maandamano kila uchao ndio democrasia ya kweli  huku wakiishia  kuumiza watu wasio na hatia.

Vilevile Mama Kisunga ameonya  kuwa uongozi  sio fujo,  sio matusi wala vitisho kama vyama vingine vinavyodhani  bali ni uwajibikaji na kuonesha ushirikiano na raia ilikulisukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa eneo atakalokuwa akilisimamia.

Licha ya hayo amesema kuwa Chama cha Mapinduzi kimewafanya watu wawe huru, wenye amani na utulivu tangu nchi ilivyopata uhuru wake toka kwa Wakoloni, hivyo basi amewataka wananchi kuendelea kukiamini Chama hicho kwa kuwachagua wagombea hao.

Ameongeza kuwa mambo ya Tegeta ESCROW sio yakuyajadili kwa sasa maana hayana manufaa kwa mwananchi mmoja mmoja bali hata fedha hizo zikitolewa zitakuwa ni za umma hivyo si vyema wakaendelea kuumiza vichwa vyao.

Kwaupande wake mgombea wa nafasi ya mwenyekiti wa Mtaa wa Mbugani ndugu Abdallah ameyataja mambo makuu manne atakayoyafanyia kazi pindi akichaguliwa kuwa ni kuanzisha mfuko wa kitongoji, kusaidia vijana kupata mikopo ya pikipiki, kusaidia wajane na wasio jiweza na kutengeneza mifereji Ya mtaa wa Mbugani.
Wanachama wa CCM wakitoka katika kampeni za kuwanadi wagombea wa nafasi za wenyeviti wa Serikali za Mitaa
Makada wa CCM wakitoka kwenye kampeni za kuwanadi wagombea wa nafasi za wenyeviti wa serikali za Mitaa Mtaa wa mbugani Disemba 3 mwaka 2014.
Baadhi ya wagombea wa nafasi za Wenyeviti kupitia Chama Cha Mapinduzi kata ya Vwawa wakiwasalimia wananchi waliohudhulia mkutano wa kampeni zao.
Katibu Tarafa mstaafu wa tarafa ya Vwawa Justina Kisunga akiwanadi wagombea wa nafasi za Wenyeviti wa Serikali za Mitaa katika Mtaa wa Mbugani kata ya vwawa, Disemba 3 mwaka huu.
Makada wa CCM wakisakata rumba katika kampeni za uchaguzi wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa zilizofanyika Disemba 3 mwaka huu kitongoji cha Mbugani -Vwawa
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika kampeni za uchaguzi wa wenyeviti wa Serikali za Mitaa kitongoji cha Mbugani kata ya Vwawa

Tuesday, 2 December 2014

UNYAYO WA MTU WA KALE

Inasadikika kuwa huu ni moja ya unyayo wa mtu wa kale eneo la Nkangamo wilayani Momba ikiwa ni moja ya vivutio lukuki vinavyo patikana wilayani humo.

UYOGA MDOGO

Uyoga mdogo (Ulunyaswa ) ikiwa ni chakula kizuri cha asili kinachopatikana maeneo mengi mkoani Mbeya na maranyingi huota kwa wingi maeneo yenye asili ya vichuguu.

MICHORO YA WATU WA KALE

Michoro ya watu wa kale iliopo Nkangamo Wilayani Momba, ikiwa moja ya vitu peekee vinavyo tunza kumbukumbu ya vitu vya kihistoria wilayani humo.

Sunday, 21 September 2014

Kimondo tours

 Waziri wa kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza akisalimiana na Mkurugenzi wa Wilaya ya Momba, Anton Mwantona
 Waziri Christopher Chiza akisomewa taarifa kuhusu mradi wa umwagiliaji wa katika kijiji cha Iyendwe kilichopo katika Kata ya Kapele, Wilaya ya Momba.
Sehemu ya ukuta wa banio la maji lililoharibiwa na msukumo wa maji katika mradi wa umwagiliaji wa Iyendwe

Monday, 8 September 2014

News and Events



Waziri Eng. Chiza akisalimiana na uongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya ya Momba

Wednesday, 3 September 2014

Contact Us

Ndama hawa wana umri wa mwaka mmoja. Ndama mwenye umbile kubwa ametokana na dume Borani na     mwenye umbile dogo ametokana na dume la ng'ombe wa asili.

Mashine ya CD4 iliyoibiwa katika kituo cha afya cha Tunduma yapatikana Zambia


Timu ya Afya iliyohusika kufuata mashine ya CD 4 Lusaka mara baada ya kufika katika makao makuu ya Wilaya ya Momba

Tuesday, 2 September 2014

MAANDALIZI YA KAZI

Mtaalamu wa mitambo akiendelea na maandalizi ya kutengeneza comedy inayoitwa "SIAMINI"