Wednesday, 30 September 2015

Picha

Wakazi wa mji wa Tunduma wakimsikiliza mgombea wa kiti cha ubunge CHADEMA  Frank Mwakajoka eneo la stendi kuu  Tunduma

Picha

Mgombea ubunge jimbo la Tunduma akiwa kwenye kampeni eneo la Stendi Kuu mjini humo

Tunduma

Mwakajoka ajifananisha na profesa

 Mgombea wa ubunge jimbo la Tunduma kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  Frank Mwakajoka ametoa kali ya mwaka baada ya kusema kuwa, mwaka huu ni mwaka wa darasa la wengi kwenda bungeni.

Mgombea huyo alisema kauli hiyo Septemba 28, mwaka huu eneo la Stendi Kuu mjini Tunduma wakati akihutubia mamia ya wakazi wa mji huo  ambao wengi wao walionesha kuipata  vema kauli hiyo kwa kushangilia na wachache tukishindwa kuelwa alichokimaanisha.

Mwakajoka alisema kuwa katika masuala ya kiutendaji kwa wananchi yeye ni profesa hawezi kubabaishwa na elimu za watu.

‘’kwa kiasi kikubwa ninajua ni namna gani ninaweza kuwaongoza wananchi wangu, na ninamna gani ninaweza kupandisha mapato ya mji wangu hivyo basi mimi ni profesa’’ alisema Mwakajoka.

Mgombea huyo aliwaahidi wananchi wa Tunduma kuwa, atakuwa muwakilishi bora wa wananchi katika bunge, na anatambua kuwa watu wake wanapenda vitu bora hivyo ataifanya kazi hiyo kwa moyo wote.

Sanjari na hayo  Frank Mwakajoka alisema kuwa katika kuinua elimu atahakikisha mshahara wake wakwanza anatangaza motisha kwa walimu wa mji huo watakao faulisha vizuri ili kuipandisha elimu katika mji wa Tunduma.

Aliongeza kuwa ataanzisha mfuko wa elimu katika mji wa Tunduma ambapo kuna wadau wengi wa mji huo wanaoweza kuchangia mfuko huo ambao utasaidia katika kutatua changamoto zilipo katika sekta ya elimu mjini tunduma.

Hata hivyo Mwakajoka aliongeza kuwa akichaguliwa kuwa mbunge atahakikisha anamshawishi waziri wa elimu kujenga chuo cha ufundi katika mji wa Tunduma ili wanao hitimu darasa elimu ya msingi na sekondari waweze kupata ujuzi ili wajiajiri.

Enea Mwanja



Monday, 14 September 2015

picha

Agrey Mwakisole mjumbe wa kamati ya siasa CCM, akiwahutubia wananchi wa jimbo la Vwawa, Mkutano uliofanyika stendi ya Malori Vwawa mjini.

picha

Wananchi wa Vwawa wakisikiliza sera za wagombea wa CCM maeneo ya stendi ya malori mjini Vwawa-Mbozi

Picha

Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi wakiwa kwenye kampeni mjini Vwawa  Septemba 14  mwakja huu

Thursday, 3 September 2015

Wanawake wahimizwa kupigania elimu

                               Wanawake wahimizwa kupigania elimu
 Wanawake nchini wametakiwa kuwa na umoja na mshikamano ili kutokomeza mifumo kandamizi  inayo zorotesha maendeleo yao katika jamii hususani suala la elimu.

Wito huo ulitolewa jana na mwanaharakati wa masuala ya kijinsia, Profesa Amina Mama katika tamasha la jinsia 2015 lililo andaliwa na TGNP Mtandao nakufanyika katika ofisi za TGNP Mtandao  jijini Dar es Salaam.

Profesa Mama alisema kuwa kutokana na tafiti mbalimbali walizofanya zimeonesha kuwa bado suala la elimu kwa mwanamke halijapewa kipao mbele hivyo wanawake hawanbudi kufanya vuguvugu la kuipa serikali msukumo ilikuleta mabadiriko katika mifumo yote kandamizi.

‘’Kitu cha msingi cha kusisitiza ni suala la elimu, wanawake lazima tufanye mavuguvugu ili kuipa msukumo serikali kuleta mabadiliko katika mifumo kandamizi’’ alisema profesa Mama.

Hata hivyo, Amina Mama aliwapongeza TGNP Mtandao kwa jitihada zao katika kupigania haki za wanawake na watu walio katika makundi maalum kwa kuandaa matamasha na warsha mbalimbali kila mwaka zinazo lenga kutoa elimu kwa jamii dhidi ya mifumo kandamizi.

Pia katika tafiti zake kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo tafiti aliyoifanya nchini Nigeria  hivi karibuni juu ya utekaji ya wanafunzi 300, ambapo utafiti huo ulionesha licha ya wananchi kuandamana kutaka wanafunzi hao warudishwe lakini serikali ilionekana kuto tilia mkazo suala hilo.

Profesa huyo alieleza kuwa, ili kufanya mabadiliko ya kweli, wanawake wanapaswa kupaza sauti zao kwa pamoja kuikumbusha serikali kutekeleza sera zilizowekwa zinazotetea wanawake, watoto na watu wa makundi maalum.

Sanjari na hayo, katika tamasha hilo linaloendelea lililoshirikisha wanaharakati kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini, zinatolewa warsha mbalimbali juu umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike, afya ya uzazi, huduma ya maji safi na salama na ushiriki wa mwanamke katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu

Wanaharakati hao waliaswa kufanya mavuguvugu maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vijijini  hata kufikia ngazi ya kitaifa kwani mabadiliko yanayo hitajika ni yale yanayoanza kwenye mizizi
Enea Mwanja.


Tuesday, 1 September 2015

Uzinduzi wa ilani ya uchaguzi TGNP

Uzinduzi wa ilani ya uchaguzi TGNP

Dar es salaam.Wanawake nchini Tanzania wametakiwa kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa uchaguzi ili wajikwamue katika mfumo kandamizi, uliojengeka kwa kiasi kikubwa katika jamii.

Tamko hilo lilitolewa na kaimu mwenyekiti  wa Chama cha waandishi wa habari wanawake nchini Tanzania TAMWA  Eddah Sanga wakati akizindua ilani ya uchaguzi  ya mtandao wa wanawake, uliofanyika Septemba mosi jijini Dar es Salaam.

Sanga alisema  kuwa ili wanawake waweze kufikia malengo ya asilimia hamsini kwa hamsini ni lazima wachague Kiongozi ambaye anaelewa matatizo yao na atakayeonesha njia sahihi ya kutatua matatizo hayo.
“Ili wanawake tufikie malengo ya asilimia hamsini kwa hamsini nilaziwa tuchague kiongozi ambaye anaelewa matatizo ya wanawake.”
Hata hivyo, Eddah aliongeza kuwa wanawake ni zaidi ya  asilimia 51 ya wakazi wote  wa Tanzania  na  wana majukumu kubwa la  kifamilia, kijamii na Taifa kwa ujumla hivyo wana kila sababu ya kushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi wa Taifa.
 Kwa upande wake Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Lillian Liundi  alisema kuwa lengo la Tamasha la mwaka  huu ni kuwasisitiza  wanawake kufanya maamuzi sahihi  katika uchaguzi mkuu,2015.

Awali kabla ya kuzinduliwa kwa ilani hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya mtandao wa jinsia nchini Tanzania(TGNP) Asen Muro alitoa historia fupi ya tamasha la jinsia ambalo hufanyika kila baada ya miaka mitatu katika viwanja vya TGNP Mabibo ambapo kwa mwaka huu limeanza Septemba mosi na litafikia tamati Septemba nne. 

Ilani ambayo imezinduliwa inasema kuwa Agenda ya Mwanamke, Turufu ya ushindi 2015 ikiwa ni tamko la pamoja la mtandao wa wanawake na katiba  na uchaguzi kutoka mashirika mbalimbali na mitandao , vikundi vya kijamii zaidi ya 65 chini ya uratibu wa TGNP mtandao.

Wanaharakati hao kwa pamoja wanaamini mfumo dume kama ilivyo kwa mifumo yote kandamizi hauwezi ukajenga mazingira ya kidemokrasia endelevu, wala hauwezi kupunguza au kuondoa umaskini.
  
 Enea Mwanja-Dar es salaam