Friday, 1 May 2015

KIKAO-MOMBA



 KIKAO CHA BALAZA LA MADIWANI -MOMBA

Mkuu wa wilaya ya Momba Richard Mbeho  amewataka viongozi wote wa wilaya hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano ili kurahisisha mfumo  ambao utawaletea wananchi maendeleo.

Mkuu huyo ambaye ana mwezi mmoja tangu aanze kufanya kazi wilaya hiyo aliyasema hayo jana kwenye kikao cha balaza la madiwani wilaya ya Momba, ambapo alisema kuwa viongozi wana kazi ya kuwatumikia wananchi kwani wao ndiyo walio wapa dhamana hiyo.

Hata hivyo aliwapongeza madiwani wa wilaya Momba  nakusema kuwa hali sio mbaya ya maendeleo, lakini kila kiongozi afanye tathimini kuwa mambo mangapi ameyafanya kwa wananchi kwaajili ya kuwaletea maendeleo.

Licha ya hayo bwana Mbeho alikumbusha  kuwa viongozi wahakikishe wanawahamasisha wananchi walio na umri kuanzia miaka 18 wajitokeze kwenda kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, ili wapate haki yao ya msingi ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu.

Miongoni mwa hayo, mkuu huyo alisema kuwa viongozi wahakikishe  wananchi wana fanya shughuli zao za kawaida na kutumia fursa zilizopo ilikupata maendeleo makubwa kwa kipindi kifupi katika hali ya utulivu na amani.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti  wa baraza hilo alisema kuwa ameipokea hotuba ya mkuu wa wilaya kwa mikono miwili , na wao kama viongozi watayafanyia kazi yote kwa kushirikiana na wataalamu wao na watafanya kazi kwa ari

Sanjari na hayo mwenyekiti wa halimashauri wilaya ya momba Benard Sichilongwa aliwaasa madiwani wa Wilaya hiyo kuwahimiza wananchi wao  kutunza chakula ili kukabiliana na suala la njaa linalohofiwa kujitokeza.

Vile vile kwa upande wa mjumbe mmoja ndani ya baraza hilo aliuliza swali kuhusu uwezekano wa kulipwa kwa wenyeviti wa vijiji, lililo jibiwa na mkurugenzi wa wilaya hiyo Christopher Eneriko kuwa kukiwepo kwa uwezekano wa kulipwa watalipwa na usipo kuwepo uwezekano hawata lipwa.

Hata hivyo kwa upande wake Sapali ambaye ni  diwani wakata ya  kamsamba alihoji kuhusu suala la chanjo ya kichaa cha mbwa ambapo alisema kuwa idara inachangia vipi kuhakikisha wananchi wanaofuga mbwa wanaipata chanjo hiyo kwaajili ya mifugo yao ilikuepusha madhara kwa watakoumwa na mbwa.

Katika kujibu swali hilo mtaalamu wa mifugo wilaya ya Momba Deo aliahidi kufuatilia suala hilo, sanjari na  kutoa elimu kwa wananchi na kusema kuwa suala la madawa  wameachiwa watu binafsi na sio la halmashauri hivyo basi wananchi waelimishwe na wawewananunua madawa kawaajili ya kuchanja mifugo hata ikitokea serikali imesaidia iwe tayari wamechukua hatua kwa usalama wao.

Na Enea Mwanja.

No comments:

Post a Comment