Thursday, 4 December 2014



KAMPENI ZA UCHAGUZI WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA CHAMA CHA CHADEMA KATA YA VWAWA

Ikiwa serikali imezindua rasmi kampeni za uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa Disemba Mosi mwaka huu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeanza rasimi  kampeni  hizo za kuwanadi  wagombea wao .

Katika mkutano huo Katibu Mwenezi wa chama hicho Emmanuel Zambi amewataja wagombea wanafasi za wenyeviti kuwa ni Medelina Nyondo Mtaa wa Haloli, Naomi Mwakasege Mtaa wa Vwawa kati, Elizabeth Kalago, Abrahamu Kalonge Mtaa wa Mwenge , John Mkondya Vwawa Sokoni , na Ephraim Mwakateba  mtaa wa Lami.

Emmanuel Zambi amewanadi wagombea hao kuwa ni wachapakazi na wamepewa mafunzo maalumu kuhusu serikali za mitaa na jinsi ya kuongoza serikali za mitaa kwa nia ya kuleta maendeleo pindi watakapopewa ridhaa ya kuongoza mitaa yao.

Vilevile kwa upande wake diwani wa kata ya Vwawa Richard Kibona amesema kuwa mji wa Vwawa unapanuka kwa kasi sana hivyo unahitaji miundo mbinu iliyo bora inayoweza kukukidhi viwango vya mji ilikuleta maendeleo katika mji huo kuliko hivi sasa

Kwa upande wake Dr Mgalla amesisitiza kuwa kwakipindi hiki mabadiriko ni lazima hivyo wasifanye makosa kuto kukichagua chama hicho kwasababu  kinalengo la kuwaletea mabadiriko ya hali ya juu kuliko ilivyo sasa.

 Katibu huyo ameongeza kuwa  miundombinu duni iliopo katika mji huo inasababisha ajali kila kukicha hivyo basi imefika kipindi cha mabadiriko wananchi kufanya uchaguzi ulio sahihi cha kuchagua wagombea wao.

Vilevile ndugu Amanyisye amesema kuwa michango yote inayotolewa na wananchi inatakiwa kujua idadi ya wananchi waliochangia na pesa zilizopatikana katika uchangiaji huo ilikuwabana viongozi wenye tamaa na pesa za walipakodi kwasababu kunabaadhi ya viongozi waliotafuna tayari pesa hizo .


No comments:

Post a Comment