Wednesday, 3 December 2014


KAMPENI ZA UCHAGUZI WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA CHAMA CHA MAPINDUZI KATA YA VWAWA
Ikiwa serikali imezindua rasmi kampeni za uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa Disemba Mosi mwaka huu Chama cha Mapinduzi (CCM) hakikubaki nyuma nacho kimeendelea na kampeni  za kuwanadi  wagombea wao zilizofanyika Tarehe 3 Disemba 2014, eneo la Ichenjezya Kitongoji cha Mbugani .

Akizungumza katika kampeni hizo katibu Tarafa mstaafu wa Vwawa Justina Kasunga amewanadi wagombea wa nafasi za wenyeviti wa mitaa kuwa ni wachapakazi na wamelelewa katika maadili ya uongozi bora hivyo wananchi wasifanye makosa kuto kuwachagua wenyeviti hao.

Aidha amesema kuwa anasikitika sana wanachama wavyama pinzani kugeuza dhana ya vyama vingi  wakidhani kupinga na kufanya maandamano kila uchao ndio democrasia ya kweli  huku wakiishia  kuumiza watu wasio na hatia.

Vilevile Mama Kisunga ameonya  kuwa uongozi  sio fujo,  sio matusi wala vitisho kama vyama vingine vinavyodhani  bali ni uwajibikaji na kuonesha ushirikiano na raia ilikulisukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa eneo atakalokuwa akilisimamia.

Licha ya hayo amesema kuwa Chama cha Mapinduzi kimewafanya watu wawe huru, wenye amani na utulivu tangu nchi ilivyopata uhuru wake toka kwa Wakoloni, hivyo basi amewataka wananchi kuendelea kukiamini Chama hicho kwa kuwachagua wagombea hao.

Ameongeza kuwa mambo ya Tegeta ESCROW sio yakuyajadili kwa sasa maana hayana manufaa kwa mwananchi mmoja mmoja bali hata fedha hizo zikitolewa zitakuwa ni za umma hivyo si vyema wakaendelea kuumiza vichwa vyao.

Kwaupande wake mgombea wa nafasi ya mwenyekiti wa Mtaa wa Mbugani ndugu Abdallah ameyataja mambo makuu manne atakayoyafanyia kazi pindi akichaguliwa kuwa ni kuanzisha mfuko wa kitongoji, kusaidia vijana kupata mikopo ya pikipiki, kusaidia wajane na wasio jiweza na kutengeneza mifereji Ya mtaa wa Mbugani.

No comments:

Post a Comment