Tuesday, 1 September 2015

Uzinduzi wa ilani ya uchaguzi TGNP

Uzinduzi wa ilani ya uchaguzi TGNP

Dar es salaam.Wanawake nchini Tanzania wametakiwa kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa uchaguzi ili wajikwamue katika mfumo kandamizi, uliojengeka kwa kiasi kikubwa katika jamii.

Tamko hilo lilitolewa na kaimu mwenyekiti  wa Chama cha waandishi wa habari wanawake nchini Tanzania TAMWA  Eddah Sanga wakati akizindua ilani ya uchaguzi  ya mtandao wa wanawake, uliofanyika Septemba mosi jijini Dar es Salaam.

Sanga alisema  kuwa ili wanawake waweze kufikia malengo ya asilimia hamsini kwa hamsini ni lazima wachague Kiongozi ambaye anaelewa matatizo yao na atakayeonesha njia sahihi ya kutatua matatizo hayo.
“Ili wanawake tufikie malengo ya asilimia hamsini kwa hamsini nilaziwa tuchague kiongozi ambaye anaelewa matatizo ya wanawake.”
Hata hivyo, Eddah aliongeza kuwa wanawake ni zaidi ya  asilimia 51 ya wakazi wote  wa Tanzania  na  wana majukumu kubwa la  kifamilia, kijamii na Taifa kwa ujumla hivyo wana kila sababu ya kushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi wa Taifa.
 Kwa upande wake Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Lillian Liundi  alisema kuwa lengo la Tamasha la mwaka  huu ni kuwasisitiza  wanawake kufanya maamuzi sahihi  katika uchaguzi mkuu,2015.

Awali kabla ya kuzinduliwa kwa ilani hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya mtandao wa jinsia nchini Tanzania(TGNP) Asen Muro alitoa historia fupi ya tamasha la jinsia ambalo hufanyika kila baada ya miaka mitatu katika viwanja vya TGNP Mabibo ambapo kwa mwaka huu limeanza Septemba mosi na litafikia tamati Septemba nne. 

Ilani ambayo imezinduliwa inasema kuwa Agenda ya Mwanamke, Turufu ya ushindi 2015 ikiwa ni tamko la pamoja la mtandao wa wanawake na katiba  na uchaguzi kutoka mashirika mbalimbali na mitandao , vikundi vya kijamii zaidi ya 65 chini ya uratibu wa TGNP mtandao.

Wanaharakati hao kwa pamoja wanaamini mfumo dume kama ilivyo kwa mifumo yote kandamizi hauwezi ukajenga mazingira ya kidemokrasia endelevu, wala hauwezi kupunguza au kuondoa umaskini.
  
 Enea Mwanja-Dar es salaam


                                                                                                                 

No comments:

Post a Comment