Wednesday, 30 September 2015

Tunduma

Mwakajoka ajifananisha na profesa

 Mgombea wa ubunge jimbo la Tunduma kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  Frank Mwakajoka ametoa kali ya mwaka baada ya kusema kuwa, mwaka huu ni mwaka wa darasa la wengi kwenda bungeni.

Mgombea huyo alisema kauli hiyo Septemba 28, mwaka huu eneo la Stendi Kuu mjini Tunduma wakati akihutubia mamia ya wakazi wa mji huo  ambao wengi wao walionesha kuipata  vema kauli hiyo kwa kushangilia na wachache tukishindwa kuelwa alichokimaanisha.

Mwakajoka alisema kuwa katika masuala ya kiutendaji kwa wananchi yeye ni profesa hawezi kubabaishwa na elimu za watu.

‘’kwa kiasi kikubwa ninajua ni namna gani ninaweza kuwaongoza wananchi wangu, na ninamna gani ninaweza kupandisha mapato ya mji wangu hivyo basi mimi ni profesa’’ alisema Mwakajoka.

Mgombea huyo aliwaahidi wananchi wa Tunduma kuwa, atakuwa muwakilishi bora wa wananchi katika bunge, na anatambua kuwa watu wake wanapenda vitu bora hivyo ataifanya kazi hiyo kwa moyo wote.

Sanjari na hayo  Frank Mwakajoka alisema kuwa katika kuinua elimu atahakikisha mshahara wake wakwanza anatangaza motisha kwa walimu wa mji huo watakao faulisha vizuri ili kuipandisha elimu katika mji wa Tunduma.

Aliongeza kuwa ataanzisha mfuko wa elimu katika mji wa Tunduma ambapo kuna wadau wengi wa mji huo wanaoweza kuchangia mfuko huo ambao utasaidia katika kutatua changamoto zilipo katika sekta ya elimu mjini tunduma.

Hata hivyo Mwakajoka aliongeza kuwa akichaguliwa kuwa mbunge atahakikisha anamshawishi waziri wa elimu kujenga chuo cha ufundi katika mji wa Tunduma ili wanao hitimu darasa elimu ya msingi na sekondari waweze kupata ujuzi ili wajiajiri.

Enea Mwanja



No comments:

Post a Comment