Wanawake wahimizwa kupigania elimu
Wanawake nchini wametakiwa kuwa na umoja na
mshikamano ili kutokomeza mifumo kandamizi
inayo zorotesha maendeleo yao katika jamii hususani suala la elimu.
Wito
huo ulitolewa jana na mwanaharakati wa masuala ya kijinsia, Profesa Amina Mama
katika tamasha la jinsia 2015 lililo andaliwa na TGNP Mtandao nakufanyika
katika ofisi za TGNP Mtandao jijini Dar
es Salaam.
Profesa
Mama alisema kuwa kutokana na tafiti mbalimbali walizofanya zimeonesha kuwa
bado suala la elimu kwa mwanamke halijapewa kipao mbele hivyo wanawake
hawanbudi kufanya vuguvugu la kuipa serikali msukumo ilikuleta mabadiriko
katika mifumo yote kandamizi.
‘’Kitu
cha msingi cha kusisitiza ni suala la elimu, wanawake lazima tufanye mavuguvugu
ili kuipa msukumo serikali kuleta mabadiliko katika mifumo kandamizi’’ alisema
profesa Mama.
Hata
hivyo, Amina Mama aliwapongeza TGNP Mtandao kwa jitihada zao katika kupigania
haki za wanawake na watu walio katika makundi maalum kwa kuandaa matamasha na
warsha mbalimbali kila mwaka zinazo lenga kutoa elimu kwa jamii dhidi ya mifumo
kandamizi.
Pia
katika tafiti zake kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo tafiti aliyoifanya
nchini Nigeria hivi karibuni juu ya
utekaji ya wanafunzi 300, ambapo utafiti huo ulionesha licha ya wananchi
kuandamana kutaka wanafunzi hao warudishwe lakini serikali ilionekana kuto
tilia mkazo suala hilo.
Profesa
huyo alieleza kuwa, ili kufanya mabadiliko ya kweli, wanawake wanapaswa kupaza
sauti zao kwa pamoja kuikumbusha serikali kutekeleza sera zilizowekwa
zinazotetea wanawake, watoto na watu wa makundi maalum.
Sanjari
na hayo, katika tamasha hilo linaloendelea lililoshirikisha wanaharakati kutoka
mikoa mbalimbali hapa nchini, zinatolewa warsha mbalimbali juu umuhimu wa elimu
kwa mtoto wa kike, afya ya uzazi, huduma ya maji safi na salama na ushiriki wa
mwanamke katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu
Wanaharakati
hao waliaswa kufanya mavuguvugu maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na
vijijini hata kufikia ngazi ya kitaifa
kwani mabadiliko yanayo hitajika ni yale yanayoanza kwenye mizizi
Enea Mwanja.
No comments:
Post a Comment