Saturday, 17 October 2015

Habari

Kinana: Wapinzani mkipata mgombea urais mwenye sifa nitamnadi

Wananchi wa vyama vya  upinzani wameombwa kuendelee kulipa ada za vyama vyao kwani  kwasasa hawana mgombea mwenye sifa za kushika  nchi.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana alipokuwa akimnadi mgombea wa uraisi kupitia chama hicho Dr. John Mgofuli, kwa wananchi wa 
Jimbo la Vwawa wilayani Mbozi.

‘’ Kwasasa mgombea mzuri anatoka CCM  hivyo  hamnabudi kumpa kura zenu , na baadae na ninyi kwa miaka ya baadae mkipata kiongozi mzuri nitawaambia wana CCM wampe kura zote’’ Alisema Kinana.

Akiendelea kumnadi mgombea huyo  Kinana alisemakuwa Magufuli amekuwa waziri kwa miaka ishirini hajawahi kupata kashfa yoyote, wala hajawahikufukuzwa hivyo basi ni kiongozi mwadilifu na hodari.

Sambamba  na hayo, katibu mkuu huyo alitumia nafasi hiyo kuwaambia wananchi wa Vwawa kuwa Wizara ya Ujenzi aliyokuwa akiishikiria Dr. Magufuri inapokea pesa nyingi lakini hakuwahi kushawishika kupokea rushwa kwenye  wizara hiyo.

Hakuishia hapo,  Abdulrahman Kinana aliongezakuwa Mgombea wa uraisi kupitia CCM Dr Magufuli ni mtu mkweli, mtekelezaji na msimamizi mzuri na endapo watamchagua maendeleo yatapiga hatua wakishirikiana na watendaji wengine.

Licha ya hayo, Katibu Mkuu huyo alisema kuwa anawashangaa wagombea wa upinzani kwani wamekaa serikalini zaidi ya miaka arobaini nao wanathubutu kuisema serikali kama haijafanya chochote.

‘’Nawashangaa sana wagombea wa upinzani waliokaa zaidi ya miaka arobaini wanaothubutu kuisema serikali kwani wao hawakuwa viongozi basi hawana sifa za kugombea maana nao hakuna walichokifanya’’ Alisema Kinana.

Aliwataka wananchi wa Jimbo la Vwawa wapime  kuwa  mtu aliye kaa serikalini miaka mingi  anawaahidi watanzania neema kwa miaka mitano  alikuwa anafanya nini kwa miaka yote aliyokuwa ndani ya mfumo.

Hata hivyo  Abdulrahman Kinana alikiri lazima wakubali wakati wa mabadiriko umefika lakini mabadiriko hayawezi kuletwa na mtu  wa umri ulio kwenda na aliyeitwa majina yote mabaya bali mtu safi na mchapakazi.

‘’Unakuja kuleta mabadiriko umri wako wenyewe ni saa kumi na mbili jioni neema gani utakayo waletea watanzania kwa muda huo’’ Alisema Abdulrahman.


Mbali na hayo aliwakumbusha wananchi wa Jimbo la Vwawa kuwa wafanye kazi kwa bidii wasipotoshwe na kauli za wanasiasa kwani  hakuna atakaye apishwa muda huohuo na akaleta bodaboda asubuhi  maendeleo bila jasho ni kazi bure.

 Enea Mwanja

No comments:

Post a Comment