Maandamano ya kukurupuka Tunduma
mwisho
Mgombea wa ubunge jimbo la Tunduma Mjini Frank
Sichalwe kupitia CCM ameahidikukomesha maandamano yasiyokuwa na kibali katika
mji huo ili wananchi waweze kufanya biashara zao kwa amani.
Sichalwe aliyasema hayo
jana wakati akijinadi kwa wananchi wa kata ya Sogea mjini humo.
‘’Tunduma ni Mji wa
kibiashara nitaulinda na kamwe siwezi kuufanya kuwa Mji wa machafuko, sitakuwa
chanzo cha kufunga biashara zenu hata kwa saa moja kwasababu ya maandamano’’.Alisema
Sichalwe.
Mgombea huyo alifafanua
kuwa maandamano ni haki ya msingi kwa kila mtanzania, lakini maandamano yana utaratibu
wake lazima yapate kibali kutoka polisi, ili wananchi waweze kufikisha ujumbe
kwa serikali yao kwa amani.
Frank aliwasihi wananchi wa Tunduma kuwa, wasitumiwe kama
daraja la uvunjifu wa amani kwani viongozi wa juu wa vyama vya siasa ni marafiki na
muda mwingi wanakuwa pamoja iweje wanatunduma wawekeane uhasama kwaajili
ya vyama.
Enea Mwanja
No comments:
Post a Comment